Safari yangu Kitaaluma.

Mwaka wa 2003,Nilikua miongoni mwa wanahabari walioteuliwa kusoma habari  za lugha ya kiswahili katika kituo cha Sayare Radio na Runinga mjini Eldoret.Kikosi yicho nakikumbuka vizuri Sana.Beatrice Gatonye ni msomaji habari KBC Channel 1,Eva Kiptoo ni mwanahabari mjini Nakuru,Scholastica Biwot na Stainley Sugut wasomaji habari Chamge fm,Jackton Omusi Hope Fm,Steve Maguta na Pamela Afandi.Safari ilianza.Nilirejea chuoni na Kuendeleza tajriba ya uanahabari na kwa mapenzi ya mwenyezi Mungu nikapata fursa adimu ya kujiunga na kitengo cha habari Cha makamu wa Rais wakati huo Mheshimiwa Moody Awori, Kakangu Shisia Wasilwa asante kwa kunitia moyo,nilipata fursa adimu kuripoti habari za makamu wa Rais maana kitengo cha Kiswahili kilitumia wanafunzi kusoma habari (interns),habari hizo zilipeperushwa katika kituo Cha Runinga KBC,nilifurahi kusikikika KBC mwaka 2005 mzoefu Badhi Muksin akisoma habari,siasa za chungwa na ndizi zilinoga nikiwa VPPS,nilitangamana na weledi wengi Pale BH nilifurahi,kuonana nao uso kwa uso na kuketi sako Kwa bako nao.Miongoni mwa watangulizi wangu Pale VPPS tulivyopenda kusema,magwiji Sasa katika jukwa hili la habari Wasilwa Shisia BBC Kiswahili ,Davis Ojiambo Radio Jambo ,Paul Nabiswa wa KTN Kenya.Wanafunzi ambao nilipatana nao wakihariri na kuripoti habari za Kingereza dadangu Kaindi Mitau,Lillian Kiilu mhariri wa video Citizen TV Kenya,na baadae wakajiunga nasi Grace Mwandware,Ronald Mutie wa Radio China Kimataifa,na wengine. Mapenzi yake Mungu nafasi ilibisha nijiunge na KTN fursa ya kujifunza jukwa kuu.Hayo maji makuu si mchezo waliopitia KTN watakueleza si rahisi kuingia KTN ukipata fursa wewe ni Bora, baada ya kufaulu kwenye mahojiano mwaka 2006 Septemba fursa nilijaliwa hilo aliyefaulu nami Johanna Chacha.Nilipenda maisha ya Runinga na mazingira hayo niliyamezea mate,siku zote nilipotumwa na aliyekua akianda habari za makamu Rais (producer) Kennedy Waziri na Justus Keesi Nilipendezwa na studio za KTN,NTV,KBC,CITIZEN.Pale KTN nilifurahi kuonana na wachapa kazi Waziri wa ardhi Bi Farida Karoney,Bwana Nzile,Bwana Ondeko Aura,Bi Mercy Oburu, Mark Wellingtone Nyongesa,Alex Chamwada,Swale Mdoe,lakini nikajenga urafiki wa karibu na Bwana Kizito Namulanda aliyekuwa Producer wakati huo na mwenda zake Ahmed Darwesh aliyenitia moyo nisikate tamaa,katika Safari yangu kitaaluma.

#Getinspired #CantonaJosephMotivates


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment