Riziki lako lipo,si mda mrefu utacheka.

Unaweza kuwa na neema ya kupata Elimu lakini kila ukitafuta kazi hupati,unaweza ukawa na pesa lakini kila ukiwekeza hazitoi faida ni hasara tu.Mungu aliumba mwanandamu tofauti na aliweka karama tofauti kwa kila mmoja,Sauli alikua anachunga punda kumbe Mungu kaweka ufalme ndani yake,Daudi alikua akilinda mifugo kondeni mungu alikua anamwandaa kuwa mfalme,Yusufu na matatizo aliyokumbana nayo alikua waziri mkuu mtarajiwa, hata wewe ni hivyo Mungu kaweka kitu kikubwa sana ndani mwako wacha kutumia akili yako.Enenda na mapenzi ya Mungu.Alikujua kabla ya misingi ya dunia,Chakarika kushoto kulia,endelea kutia bidii,hangaika Kila pembe.Riziki lako lipo,si mda mrefu utacheka.
Maneno ya watu yanaweza kufanya ukachoka kabisa na kukutisha ukaona haiwezekani tena kutoka kwenye shida uliyo nayo,Yupo Mungu anayeishi yeye huondoa udhaifu wote na atakutenga mbali na kuonewa.Kuanzia leo uwe huru,neno hili likawe mkate na maji likakupe nguvu ya kuanza na kusonga mbele.Ni maombi yangu kwako hakuna wa kukushinda tena.Wengi tuna ushuhuda umbali mungu ametuleta.Ndio maana tunaushujaa, kulitangaza neno la Bwana Yesu, Kimbia mbio kila siku ukimtazama aliyekuumba mwanzilishi wa mambo mema maishani mwako.Kitabu changu Beauty Out of Brokenness kipo hatua ya mwisho mwisho kukamilika hapo ndipo utayafahamu mengi utakapokisoma kitakapochapishwa
Pokea mengi kutoka kwenye website yangu http://CantonaJoseph.wordpress.com
#CantonaJosephMotivates. #Iposiku #Getlnspired #Itissettled


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment