Mungu hujibu hitaji letu.

Mungu hajawahi chelewa kujibu hitaji la mtu,husikia sala na maombi yako.Neno linasema yale yote tuombayo tukiwa tunasali yameshakuwa yetu (Marko 11:24).Shetani huwa anasubiri siku ambayo unakwenda kubarikiwa ukikaribia tu anakufanya ukate tamaa na kufanya uzunguke muujiza wako ni kama wana wa Israel njia ya kwenda nchi ya ahadi Mungu alikua anaijua kabisa na ilikua nyepesi sana lakini walizunguka jangwani na milimani miaka 40 kwakua walikua kila mara wanamuacha na kutenda dhambi.Ukiona ulikuwa unafanya maombi juu ya jambo fulani ukawa mkamilifu alafu kuna siku ikatokea msukumo wa kufanya dhambi ujue ndiyo siku yako ya kupokea ulicho kiomba.Unakuta siku yako ya mfungo wa mwisho wa maombi ndio makwazo yanaibuka unakasirika na ugomvi juu mpaka unashindwa kufunga usikubali shetani akutolee muujiza wako maana ukitenda dhambi tu Mungu anakua mbali na wewe utaanza moja tena kumuomba ndio maana unaona kama unachelewa kujibiwa kumbe kuna mahali umejichanganya.Nakuombea leo shetani asikutoe kwenye imani yako na kudanganya moyo wako simama katika njia sahihi na ukapokee hitaji lako.Namsambaratisha ibilisi atoke kwenye njia yako kwa Jina la Yesu.

Pokea mengi kutoka kwenye website yangu http://CantonaJoseph.wordpress.com
#CantonaJosephMotivates. #Iposiku #Getlnspired #Itissettled


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment