Kujitetea kwa kulaumu wengine kumewafanya wenye mamlaka kupoteza nafasi zao pasipo kujua. Wakati mwingine tumemkabidhi adui nguvu ya kutupiga kwa sababu tu TULIJARIBU KUJITETEA ILI TUONEKANE TATIZO SIO SISI ILA WENGINE.
Ndicho alichofanya Adamu pia alipoulizwa kwa nini kala tunda? Akajitetea kuwa ni mwanamke ndio kasababisha, ASIJUE ANAHAMISHA NAFASI YAKE KUMPA MWANAMKE. Mungu akamgeukia mwanamke naye akafanya kosa lile lile akajitetea kwa kumlaumu nyoka( shetani).Shetani akajua sasa hii ni nafasi adimu yeye hakulaumu mwingine, akawajibika na MWANADAMU AKAMFANYA SHETANI AITWE mungu wa dunia hii kuanzia hapo pasipo kujua…. 2Kor 4:4.
Nampenda Yesu maana yeye alipoulizwa kuhusu mashtaka yake, hakujibu wala hakumlaumu mwingine maana alijua siri hii, alijijua yeye ndiye mtawala hivyo anawajibika kwa nafasi yake, hata kama alihukumiwa pasipo kuwa na hatia lakini aliiheshimu kanuni hii muhimu. KWA KUFANYA HIVYO AKAFANIKIWA KUMNYANG’ANYA SHETANI UTAWALA KWA KANUNI ILEILE.
HUHITAJI KUJITETEA KWA KULAUMU MTU MWINGINE ILI UONEKANE UNA HAKI, NYAMAZA KIMYA ILI USIMPE NAFASI ADUI YAKO KUKUTAWALA NA KUJIFANYA mungu kwako. Kimya kina majibu ya maana zaidi kuliko majibu ya sauti ya KUJITETEA kwa kulaumu wengine. Ni bora kunyamaza.
Pokea mengi kutoka kwenye website yangu http://CantonaJoseph.wordpress.com
CantonaJosephMotivates. #Iposiku #Getlnspired #Itissettled

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.