Maisha ni Kitabu ambacho kila kukicha,wino unaandika matukio,ni riwaya ambayo inasomwa, ni mchezo wa kuigiza ambapo mhusika mkuu ni mwanadamu.Namshukuru Mungu alinipa fursa adimu kuongoza wanafunzi wenzangu katika shule ya upili,nilikua kiranja anayesimamia jumba la maankuli shuleni [dining hall captain], naibu mwenyekiti wa ushirika wa wanafunzi wakristo shuleni [christian union] mwenyekiti wa chama cha kiswahili na mwenyekiti wa chama cha habari na mazingira shuleni. Nilifurahi kuhudumia wanafunzi wenzangu na kuwahutubia umuhimu wa kuishi maisha ambayo yanampendeza Mungu,kumcha Mungu kuna faida yake, kuishi kulifahamu hilo na hamna kisichowezekana maishani iwapo utamtegemea Mungu katika hatua unayoipiga.Mungu anawezabadili historia yako.
Jambo wengi sana wanaumia,katika safari hii ya maisha au wanagharamika sana, na wengine wanakufa kabisa kwa sababu tu, wanapopatwa na matatizo HAWAJUI KITU SAHIHI CHA KUFANYA.Watu wengi ndoto zao hufaa sababu ya kutokua wepesi wa kuelewa.
Sio kwamba hawafanyi kitu ila wanafanya yasiyo sahihi na mwisho wa siku wanakuja kusaidika mwishoni sana wakiwa wameshaumia, wamechoka, wamefilisika, wamechakaa na hawafai kabisa, wengine wanakufa kwa huzuni kabisa pasipo hata kusaidika.
Angalia kisa hiki cha wanawake wawili Mark 5:25 soma pia 42A
Wa kwanza alitokwa na damu miaka 12, akafanya yasiyo sahihi,kuchelewa kutambua mapema.
Akagharamika mali zake zote, kwa waganga na haikumfaa, akaja kushtuka kumtafuta Yesu akiwa ameshachoka sana, na Yesu alipomponya akamwangaliaaa akaona keshakuwa useless maana hana tena alichopaswa kuja nacho kwenye ufalme, AKAMWAMBIA NENDA ZAKO KWA AMANI ( hakumpa wajibu wowote maana hana tena kitu)
Mwingine ni binti wa mkuu wa sinagogi naye alikuwa na miaka 12 alipokufa, lakini baba yake alijua kitu sahihi cha kufanya, yeye AKAANZIA KWA YESU NA BINTI AKAFUFUKA
Hii ina maana siku mwanamke alipoanza kutokwa damu isiyokoma ndipo yule binti wa mkuu wa sinagogi alizaliwa. Bahati mbaya mwanamke akaponywa siku binti anafufuliwa baada ya miaka 12.
HAIJALISHI HALI YAKO IKOJE LEO, NAKUSHAURI UWE NACHO AMA USIWE NACHO KITU, KATIKA SHIDA YEYOTE ANZIA KWA YESU KWANZA. La sivyo unaweza ukapotea mzima bila hata kushtuka mwishoni, na wewe uliye mwishoni hujachelewa nenda kaguse pindo lake hata kama umeshachoka umechakaa BADO NI MWENYE REHEMA.
Usiogope ugumu na urefu wa mlima unaoupanda maishani endelea mbele kabisa mpaka kileleni, ukifika hapo utagundua nyuma ya mlima uliokusumbua kupanda kuna mtelemko mkali.
Unavyoumia zaidi ndivyo unavyokaribia kileleni JIKAZE UMALIZE SAFARI YA MLIMA WAKO, MAANA TUZO LIPO KILELENI VUMILIA BADO KITAMBO KIDOGO UTAFAULU,NA UTAKUA KIELELEZO CHEMA KATIKA JAMII.
Pokea mengi kutoka kwenye website yangu http://CantonaJoseph.wordpress.com
CantonaJosephMotivates. #Iposiku #Getlnspired #Itissettled


Unapomtumania Mungu unakua jasiri siku zote.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.