KANUNI YA HESHIMA

Katika maisha nimejifunza unahitaji sana watu ili ufanikiwe, na watu hao wanaweza kuwa wazazi, viongozi, boss, wachungaji au watumishi wa Mungu, marafiki, majirani nk.
Lakini wengi wetu hatujapokea baraka, vitu, maombi, heri na upendeleo kwa sababu ya KUKOSA HESHIMA KWA WATU AMBAO TUNAWAHITAJI ILA KWA KUTOJUA TUMEDHANI HATUWAHITAJI.

Umewahi jiuliza kwa nini wafanyakazi hawapokei upendeleo wa wasimamizi wao? Watoto wa wachungaji ama wake au waume wa wachungaji hawapokei yale ambayo watu baki wanapokea kwa mtu yuleyule ambaye wao wanamuona wa KAWAIDA? shida iko kwenye kutambua nafasi ya hawa watu juu ya maisha yao.

Ukinichukua Mimi nikakae kwa mchungaji wangu, kwa kuwa namheshimu nitahakikisha nafanya mazuri ambayo hata nyumbani kwangu huenda sifanyi, LENGO LANGU NIMUONYESHE NAMNA GANI NAMHESHIMU, NA BILA SHAKA ATAACHILIA MOYO WAKE NA NITAPOKEA KITU ambacho huenda watu wa familia yake wasipokee maana wanamuona ni baba wa kawaida, mama wa kawaida hivyo wanakosa sehemu ya alichonacho.

Kuna watu wawili kwenye biblia najifunza kwao, DAUDI NA ELISHA. Daudi alimheshimu sana Sauli licha ya kuwa alikuwa anamuwinda kumuua, alimuona ni masihi, alimuona ni Bwana wake ( mwisho akathibitishwa na adui yuleyule kuwa IPO siku atakuwa mfalme hakika) soma 1Sam 23 na 24 utajifunza vizuri hii kanuni.
Elisha yeye alimuona Eliya kama baba yake kwa kuwa alitambua umuhimu wa roho ya Eliya na hakumuona wa kawaida na alipopata nafasi aliomba mara dufu sehemu ya roho yake na akapokea 2 Wafalme 2

KANUNI YA KUWAFANYA WALIOTUZIDI KUACHILIA VITU NA VIKATOKEA NI KWA KUWAHESHIMU, HATA KAMA BABA YAKO, MAMA YAKO, KAKA AU DADA, MUME AU MUME UNAMUONA WA KAWAIDA NAKUSIHI USIJIDANGANYE, ANAVYO VITU UNAVYOVIHITAJI SANA, NA HUTAVIPATA MPAKA UKAJIFUNZA KUMHESHIMU ILI KUMFANYA AACHILIE KWAKO PIA KAMA ANAVYOACHILIA KWA WATU BAKI. BARIKIWA SANA.

Pokea mengi kutoka kwenye website yangu hii link http://CantonaJoseph.wordpress.com

#CantonaJosephMotivates. #Iposiku #Getlnspired #Itissettled


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment